Taifa Leo on Sept 12, 2015

Will Taifaleo

AFISA  Mkuu Mtendaji wa  mradi wa  E-Kitabu ambaye pia  ni mwasisi wake, Will Clurman azungumza wakati wa  kikao na wanahabari mjini Nairobi jana  ambapo alizindua mpango wa  masomo wa

e-learning kwa  shule za Afrika  Mashariki. Mpango wa  E-kitabu umeshirikiana na Taifa Leo/Swahilihub kuwatuza wanafunzi bora katika shindano la kidijitali la uandishi wa  insha. Picha/JEFF

ANGOTE..      Na LEONARD ONYANGO

 

WASICHANA wamebwaga wavu- lana katika shindano la uandishi wa insha za kidijitali la mwaka huu linalofadhiliwa na kampuni ya kusambaza vitabu kupitia mfumo wa kidijitali, eKitabu kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu na wadau wengineo.

Kulingana na matokeo yaliyo- tangazwa jana, wasichana kote nchini wametwaa nafasi za kwanza na pili katika vitengo

vyote vya shule za msingi na sekondari.Msichana kutoka shule ya Lo- reto  Convert Valley  Road,  Nairobi ndiye mwandishi bora  wa insha ya Kiswahili katika kitengo cha shule za msingi baada ya kuibuka na alama 80.63 huku mwenzake wa Hill School Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu akitawazwa mshindi kwa alama 82.2  katika kitengo

cha shule za upili.

Katika kitengo cha uandishi wa insha ya Kiingereza, msichana  wa shule ya Little Angels, Kaunti ya Isiolo  alitawazwa mshindi kwa kupata alama 86.9  katika kitengo cha shule za msingi. Katika kiten- go cha shule za upili, wanafunzi wa shule za Moi Girls -Eldoret, Precious Blood  Riruta- Nairobi

na Maranda, Siaya walitangazwa waandishi bora  wa insha ya Kiingereza baada ya kupata alama 87. 85 na 83 mtawalia.

“Kampuni ya eKitabu imekuwa ikiandaa shindano la uandishi wa insha kila mwaka tangu 2013. Mwaka huu tulipokea jumla ya insha 2,100 kutoka kwa wanafun- zi zaidi  ya shule 400  za kaunti 45. Hatukufanikiwa kupata insha kutoka Kaunti za Wajir  na Pokot Magharibi,” akasema Will Clurman, Mkurugenzi Mkuu wa eKitabu.

“Katika insha ya mwaka huu, wanafunzi walitakiwa kuandika barua kwa Rais wa taifa la Kenya wakimweleza kuhusu maisha

yao  kama wanafunzi wa kidiji- tali chini ya kichwa : ‘Kwa Rais Mpendwa….maisha yangu kama mwanafunzi wa kidijitali’,” aka- ongezea.

Gazeti la Taifa  Leo na tovuti ya Swahilihub wamefadhili tuzo za vipakatalishi 6 vitakavyotunuki- wa washindi watatu bora  katika kitengo cha shule za msingi naza upili.

Original Article:

Ekitabu Media breakfast (1)_001