Anderson Kithi – Malindi High School

Kwa Mpendwa Rais,

Nina furaha kuu kwa uzima na ubuheri wa afya. Matumaini yangu kwamba umzima. Pokea salamu zangu za heri na fanaka. Ningependa kuchukua fursa hii kama mwanafunzi wa wa kidijitali kukuelezea jinsi masomo yalivyoboreka shuleni mwetu kidijitali, najiona kama mgomba kwenye chemichemi ya maji tayari kunawiri.

Masomo siku hizi yamepeperushwa hewani na yeyote anayetaka kusoma basi anaweza kusoma wakati wowote, mahali popote bila hata kitabu wala kalamu. Siku hizi simu nyingi za mkononi zimeboreshwa na wavuti ndani ambapo unaweza kufungua mtandao wa ‘google’ na ukaandika swali pale ama kitu chochote kile ambacho unahitaji maelezo zaidi kukuihusu, kisha papo kwa hapo unaletewa jawabu moja kwa moja. Walimu wa lugha hawakosekani, pia wamo mitandaoni katika www.dictionary.com, utapata kamusi ya kingereza inayoeleza na pia kukupa matamshi sahihi, (Tazama paneli la kiswahili na kizuu cha binadamu katika somo la bayolojia.

Mimi hununua mjazo kwa simu kisha hununua ‘bundle’ ya intaneti; ambazo hizi ni pesa zinazoweza kutumika wakati ninataka kutukia intaneti pekee yake. Kwa mujibu huwa basi wanateknolojia wametoa vipakatalishi ambavyo vimekuza teknolojia kwa matumizi ya intaneti na wizara ya elimu pia ikaona ni heri kila shule hapa nchini kenya ipate vipatakalishi toshelezi ili wanafunzi na hata walimu ambao hawana uwezo wa kununua rununu zenye wavuti wakaweza kupata elimu hii ya kidijitali. Ndio maana somo la kopyuta likanuiwa kufunzwa katika kila shule ya upili Kenya na hata katika shule za msingi.

 

 

Ninaingia hewani, siseme ninapotea

Kompyuta mkononi, kazi inanitendea

Intaneti niko ndani, kweli nasherehekea

Nimetokea gizani, nahamia dijitali

Kwa sasa shuleni kwetu matumizi ya tarakilishi yamenoga sana kwetu sisi wanafunzi na hata wlimu. Kompyuta zimetumika katika uandishi na kuhifadhi data ambao kwa wanafunzi huwa ndio umechuka asilimia kubwa katika maisha haya ya kidijitali. Kwa sasa mimi kama mwanafunzi wa kidijitali haina haja niandike kwenye vitabu bali huandika kupitia kompyuta kisha nikimaliza kuandika nakala hiyo huihifadhi kwenye kifaa cha kuhifadhia nakala: ‘Flash Disk’ hiyo basi kumwezesha mwanafunzi kusoma popote alipo aendako na kwa wakati wowote ilimuradi tu kuwe uwepo wa kipakatilishi kwa sababu kifaa hiki cha kuhifadhia nakala mbalimbali ni wastani na unaweza kutembea nacho popote utakapo.

Shule yetu pia imedijitika sana kwa sababu wanafunzi kutoka shule nyingine hutembelea shule yetu ili kupata elimu hiyo ya kidijitali. Wanafunzi kutoka shule nyingine basi sisi ndio huchukua jukumu la kuwafundisha kuonyesha umahiri wetu katika somo hili la kompyuta.

Vile vile vipakatalishi sana walimu hasa wa Historia. Walimu hawa hutumia mitandao kama vile ‘Google na Youtube kutazama video za mambo yaliyofanyika kale kama vile vita vya kwanza na vya pili vya dunia na hatimaye huchukua video hiyo kutaka mtandaoni na kuifadhi kwa disketi ama vifaa vingine vya kuhifadhi nakala kielektroniki na mwishowe humsaidia mwalimu katika kufundisha kwa sababu wanafunzi wanapotazama kanda hiyo huwapa uwezo wa kutathmini haraka matukio yaliyotokea hapo kale.

Walimu wetu siku hizi hupeperusha mitihani ya kila mwisho wa muhula kupitia wavuti wa shule yetu; malindihighschool.ac.ke nifikapo nyumbani hufungua wavuti hiyo na kudurusa maswali yaliyomo. Pia shule yetu haipokei pesa taslimu bali wazazi wanapohitaji kutuma karo hutuma kupitia M-Pesa au kuweka kwa benki bora tu uwe na namabri ya akaunti ya shule na unapofanya hivyo basi, pesa huingia moja kwa moja kwa moja kwa shule.

Kwa sababu ulimwengu wa sasa ni wa kidijitali katika shule nyingi matumizi ya kalamu kwa chaki yamepungua kwa kiwango kikubwa sana kwa sababu walimu siku hizi hutumia kompyuta pamoja na projekta baadala ya kuandika ubaoni na chaki ambayo hata mara nyingi huzusha magonjwa mathalani pumu na kikohozi. Kwa hivyo basi ni ombi langu kama mwanafunzi wa kidijitali Bwana Raisi Uhuru Kenyatta nakuhisi kuongeza vipakatalishi shuleni ili kwa mwanafunzi aweze kupata masomo haya ya kidijitali na kuweza kuishi kidijitali: Ndio maana mwito wetu ni Soma! Soma! Tunaenda dijitali.

Tamati nimefikia, jamvi langu nalikuja

Dijitali nahamia, karibu kwenye uwanja,

E-kitabu nasifi , kwa kutoa hino hoja,

Nimetokea gizani, nahamia dijitali