Darvyne Wakarindi – Tetu Girls Primary School

Kwa mpendwa rais…….Maisha yangu kama mwanafunzi wa kidigitali.

Kwa mpendwa Rais mimi ni mwanafunzi ambaye amefurahia kazi yako kuu ya kiteknolojia. Teknologia imeweza kuwasaidia watu wengi nchini kote.

Kwanza kwa kimasomo, umetusaidia sisi wanafunzi sana kwa kuanzisha mradi wa utumiaji wa vipakatilishi katika shule zote za msingi nchini. Kabla ya nyota ya jaha ya teknolojia kutuangukia, nchi iliparara na kupauka. Nyuso za raia wa Kenya zilijaa makunyanzi na makunyato.

Hapo ndipo teknolojia iliibuka ghafla bin vu na baada ya muda tulianza kuona matukio yaliyotukiza kwa tukutiko tukutuka. Sasa, wanafunzi wanaweza kusoma bila madaftari yaliyo na uwezo mkubwa wa kuraruka raruraru. Pia mfumo huu mpya wa kidigitali unawafanya wanafunzi kumakinika kwa masomo kwani wanapata faraja kugusagusa vipakatalishi vyao.

Pili, teknolojia husaidia katika wavuti katika mtandao. Kwa mfano, ninaweza kuwasiliana na rafiki yangu aliye ughaibuni. Teknolojia kweli!……… rais, asante. Teknolojia husaidia kurahisisha kazi na utekelezaji wa shughulli katika harakati za wanadamu walio katika ulimwengu wa sasa. Teknolojia inatusaidia kutafuta majibu mengi ya kisayansi.

Tatu, teknolojia hutusaidia sisi kama raia wa Kenya kwa kupiga kura. Kura huhesabiwa haraka mithili ya chui mbioni na tunapata matokea baada ya muda mfupi. Mfumo mpya wa kidijitali umewezesha maisha yetu kuwa kama darubini. Kana kwamba tunaweza kutabiri kitakacho fanyika wakati ujao. Kwa mfano, katika hali ya anga.

Nne, teknolojia inatusaidia kupata maarifa kuhusu nchi zingine. Kwa mfano uchaguzi, sherehe za kimataifa, vita na mambo mengine. Pia inatusaidia kujua kinachoendele nchini mwetu. Kama kazi mbalimbali za serikali yako, michezo ya riadha ambayo raia wetu wa kenya walishinda.

Nyanja nyingi kama vile vilimo, viwanda, ufundi na hata mawasiliano zimenufaika kutokana na teknolojia. Hata hivyo, kama wahenga walivyo nena hakuna masika yasiyokuwa na mbu. Teknologia inazo athari zake.

Watu wengine hutumia teknologia kupitisha habari mbaya kuhusu ukabila,chuki,utengano na vita. Hata hivyo, natumai kuwa wewe rais utapigana na wote ambao wanatumia zawadihii nzuri vibaya. Asante kwa kuwa umetufunza maisha ni lengo ni lengo ni lazima tulifikie.

Tutashirikiana na wewe kwani tembe na tembe huwa mkate aidha jifya moja haliinjiki chungu. Pia tumeitambua kuwa umefanya kazi kwa moto mmoja kama chui aliyechachama na chachawa si haba. Ndiposa nakuunga mkono rais kwa kunijenga mimi kama mwanafunzi wa kidigitali.