Makena Marlene Gacheri – Loreto Convent Valley Road

Kwa Mpendwa Rais…..Maisha Yangu Kama Mwanafunzi Wa Kidijitali

Maisha yangu kama mwanafunzi wa kidijitali yatakuwa yenye furaha na kufarakana. Elimu ni taa inayong’aa na kuzagaa gizani. Elimu ni ile ile lakini mbinu zimerahisishwa na kuwafaa wanagenzi wote nchini mwetu. Mbinu hizi ndizo zitakazo wafanya wanafunzi wapiti mtihani yao vizuri na waweze kutimiza ndoto zao.

Teknolojia ni utumiaji wa maarifa ya sayansi yaliyowekwa katika vitu serikali ya Kenya ambayo iko chini ya mamlaka ya mheshimiwa rais Uhuru Muigai Kenyatta imezindua mbinu mpya ya kuwaelimisha wanafunzikwa njia ya teknolojia.

Teknolojia itawasaidia wanafunzi kuhifadhi elimu yao ya kila somo kwenye ngamizi kama waya wanavyofahamu fika ni kuwa, vitabu hweza kuraruka raruraru na kuliwa na wadudu kama kombamwiko anayependa kutafuna karatasi. Jambo kama hilo likitendeka wanafunzi huwa na changamoto kubwa ya kunakili tena waliyokuwa wameandika vitabuni mwao.

Kinyume na hayo, chochote kilicho hifadhiwa au kuwekwa katika ngamzi hubaki papo hapo hadi utakapokitoa wewe mwenyewe. Hii humsaidia mwanafunzi kuhifadhi masomo yake na kuweza kuyapata kwa urahisi.

Fauka ya hayo, teknolojia husaidia pakubwa shuleni. Usalama huchangia maendeleo ya shule Fulani ikiwa hakuna usalama , adinasi huishi kwa uwoga mithili ya kunguru. Hivi majuzi tumeshuhudia kisa cha ugaidi katika andaki ya Garissa. Wanafunzi gana moja arubaini na saba walifarakana na sayari ya tatu . Kama kungekuwa na ulinzi bora maisha ya insi wengi yangekuwa hai sasa lakini yaliyopita si ndwele , tugange yajaayo .

Wakati huu, nyakaso za upelelezi hutumiwa shuleni na nyaya za umeme huzingira shule . Hii huwafanya wanagenzi wadansi na wote bwaliokuwa shuleni kule kujihisi wenye usalama. Methali amani haiji ila kwa ncha ya upanga imepitiwa na wakati na kubaki nyuma ya koti la babu .Kila binadamu anapaswa kutahadhari kabla ya athari. Amani na usalama ni kiini cha utangamano na maendeleo mazuri katika jamii.

Teknolojia itawatolea wamafunzi mzigo mkubwa. Mmikoba yao huwa mizito sana nanga tupilia mbali katika kaburi ya maghafala. Vitabu vyao vya ziada huwa vingi kinyume na vipatakalishi ambavyo inshallah wanafunzi watapewa. Vipatakalishi huwa vyepesi aghalabu huwa na mizani ya kilo moja.

Takwimu zimeonyesha kuwa shanta nzito huweza kuudhuru utingili ambao huwa mojawapo za sehemu muhimu sana mwilini. Wanafunzi wakipata vipatakalishi wataweza kujinusuru kutokana na ndwele tofauti.

Vipatakalishi vitakavyopewa wanafunzi, vitatumia miale ya jua kufanya kazi. Wanafunzi wote hata wanaotoka familia  zenye ufukara wataweza kuvitumia pia hupunguza fedha ambazo zingetumika kulipia umeme. Namna hii itawafaidi waja wote.

Uzuri mwingine wa teknolojia ni kuwa, huwasaidia wanafunzi kuchambua mambo mengi yanayohusu masomo yao.Mtandao huwawezesha kujua mengi hata wakiwa wameketi chengoni mwao. Wanaweza kuzuru nchi zozote duniani na pia angani furaha iliyoje.

Elimu haina umri wala jinsia. Wavyele wa wanafunzi wa kidijitali hufaidika pia. Wao pia huweza kuchunguza maarifa mengine kuhusu ujuzi wao katika mtandao. Mathalani ikiwa mzazi ni mkulima, yeye huweza kujua na kufahamu vyema kuhusu zaraa. Yeye pia huweza kujua ni mimea ipi itakayomea vizuri. Baada ya kufuata maagizo yale, mkulima huweza kuikuza aila yake. Yeye hupata fursa ya kuwapeleka wana wake shule nzuri na kuanzisha biashara nyingine.

Teknolojia hutumika kwa mawasiliano aina mbili kama barua pepe na nyinginezo. Wanafunzi huku Kenya wataweza kuwasiliana na wanafunzi wengine huko ulaya. Wao huweza kujadiliana kuhusu mada yoyote na hueneza utangamano na umoja kati ya wanafunzi hawa. Wazee wa jadi walisema  kuwa udongo uwahi ungali mbichi. Wanafunzi wakieneza upendo wakiwa bado wachanga, watakuwa na hulka hiyo hiyo na kuwa vielelezo katika jamii zao.

Fauka ya hao, teknolojia huwa na video mbalimbali ambazo mwanafunzi huweza kuvitazama. Kwa mfano, ikiwa mwanafunzi Fulani ana kipawa cha kuimba vyema au maneno mazuri ya kumtoa nyoja pangoni , yeye huweza kutazama video za kukuza kipawa chake. Ingawa video zingine huwa chafu na zenye kushusha maadili, lazima mwanafunzi awe mwenye busara na akili safi ya kukataa  abadan katan kuzitazama ili mienendo yao mema ibaki vivyo hivyo.

Hebu tulia kidogo na kupata taswira ilivyo kuwa zamani wakati wa masomo . Wanafunzi wangepiga milundi kilomita nyingi kabla ya kuwasili shuleni na wangejaa sana hadi darasa likatapika wengine. Mwalimu alikuwa mmoja tu! Jambo hili lilikufanya kufunza kuwa shida kubwa. Kweli, mola hamsahau mja wake. Alimpa mwanadamu akili ya kuunda teknolojia ambayo imesaidia kila moja kwa njia moja au nyingine waama , Jalali ni mwema.

Mheshimiwa rais, aushi yangu kama mwanagenzi wa kidijitaliitainuka na kurahisika sana. Shukrani nyingi kwako mithili ya mchanga baharini kwa kuhusisha teknolojia katika masomo yetu.