Wafula Nasipondi Sharon – Hill School, Eldoret

Mpendwa Rais, mimi mwanafunzi wa kidigitali na mzalendo wan chi hii tukufu ya Kenya nina furaha na bashasha si haba. Kwanza kabisa, kwa moyo mkujufu ningependa kukupongeza na kukupa heko kwa kunifaa. Sio mimi tu bali hata na wanafunzi wengine wa kidigitali. Tunakuvulia kofia kwani unatuwezesha kupiga hatua kubwa na kukwea vidato vingi katika ulimwengu wa kidigitali.

Nakumbuka wakati ambapo nililazimika kubakua vitabu na hata kamusi ili kutafuta maana mwafaka ya neon moja tu. Ilikuwa inachosha kwa sababu hata vitabu hukinzana kwa njia moja au nyingine. Hivi sasa kupitia mtandao wa google nina weza kutafuta neon kwa sekunde kiduchu. Zaidi, ninaweza kutafuta tafsiri ya maneno kutoka lugha ya kiingereza hadi Kiswahili kupitia safu ya swahilihub.

Ulimwengu wa kidigitali umenipa fursa ya kukaza lugha tukufu ya Kiswahili. Imeniwezesha kujiunga na chama cha Kiswahili cha mtandao almaanifu CHAKI254. Hiki ni chama ambacho kimeniwezesha kukuza Kiswahili na hata kimenisaidia kuimarisha matokeo yangu katika somo hili. Nimejifunza mengi kuanzia lugha, misamiati na hata fasihi.

Mtu ni watu kwani mtu pekee hashui jahazi. Ulimwengu wa kidigitali umenipa jukwa ya kuzungumza na wanagenzi wengine walio katika sehemu zingine za nchi. Nimepata fursa ya kubadilishana mawazo na kujifunza mambo mengi kuhusu elimu. Haya yote kupitia mitandao ya kijamii. Waama, dunia imekuwa kijiji kidogo kwa sababu ya technolojia.

Sasa hivi ninaweza kupata vitabu vingi vya kusoma kwenye mtandao. Vitabu ambavyo vinaweza kunisaidia kuimarisha matokeo yangu. Hata hivyo, kuna kanda za vitamu za vitabu vya mtalaa kama vile kidagaa kimemwezea. Ninapozitazama filamu hizo, kuelewa kitabu hicho huwa ni rahisi sana kinyume na hapo awali. Aidha, haya yote yananinoa na kunitia makali ili niwe na ujasiri wa kukabiliana na ulimwengu nikapohitimisha kisomo changu kwani elimu bila amali ni kama nta bila asali.

Hata hivyo, wenzangu ambao wana studio za kidigitali shuleni mwao ambamo mwalimu anaweza kuwafunza wanafunzi akiwa majilisini mwake. Hivyo kumwezesha kuwafunza wanafunzi wa idadi kubwa. Hata kwake, imeimarishwa. Mojawapo wa shule hizo ni shule ya upili ya wavulana ya Kabarnet.

Rais mtukufu Huru Kenya, ningependa kukushukuru kwa kushirikiana na idara ya elimu ilikuhakikisha kwamba wadogo wetu walio katika shule ya msingi, watapata fursa ya kusoma somo la kompyuta. Hili ni wazo bora sana kwani hii ni njia mojawapoya kuwasaidia kukabiliana na mabadiliko yaletwayo na teknolojia.

Mpendwa Rais, najua unafahamu fika kuwa chungu huijikwa moto ukishawaka. Kuna wale wanafunzi ambao wameishia kutumia vibaya vyombo vya teknolojia. Mfano, kuna wanafunzi ambao hutazama filamu na picha zisizofaa licha ya umri wao mdogo kwenye mtandao. Jambo hili huzorotesha maadili na tabia ya wangezi hao. Ni nani asiye jua kuwa tabia ni kia cha mwili maadamu ni ngozi unaweza kuwa ngumu kubadilishwa?

Kando na wanafunzi mara nyingi tumeshuhudia watu ambao wanawahadaa watu kupitia mitandao na hata kuzua hafu. Kuna wale wana watishia wenzao maisha yao. Jambo ambalo si nzuri asilani kwani wao ndio wanaovuruga mambo mazuri ambayo yanaletwa na ulimwengu wa kidigitali.

Kutokana na kuletwa kwa studio za kidigitali shuleni, kuna walimu wngi ambao wataishia kulaza damu kazini. Wanafunzi hawatapata fursa nzuri ya kuigiliana na walimu wao moja kwa moja hivyo basi kuongeza pengo katika uhusiano wa walimu na wanafunzi wake moja kwa moja.

Ninasaidika kuwa kila kitu kina dosari hata mwanadamu si mkamilifu ndio maana tunastahili kuhesabu mazuri yaliyoletwa na teknolojia. Tunafaa kujifunza kutokana na na hayo kwani elimu ni bahari haina mwisho na wala sio kuwakasifu.

Kabla sijafika ukingo nina ujasiri kusema kuwa hivi sasa ni la kupendeza kuona kuwa matokeo ya mtihani ya kitaifa inapatikana mtandaoni. Hivi basi mtahiniwa halazimiki tena kwenda shuleni ili kupata matokeo yangu. Hata usijali wa watahiniwa hufanywa kidigitali. Na hayo yote ni maendeleo ya taifa.

Bila kusahau, hata mashindano haya niliyajulia mtandaoni na hata unawasilishwa mtandaoni. Kinyume na hapo awali ambapo ingenibidi nitumie anwani ya posta, sasa natumia tu baruapepe. Hata mashindano ya uandishi yameamia digitali.

Ninapafika ukingo, shukrani zangu zikuendee Rais kwani ningekuwa muwa, ningekutengenezea sukari lau ningekuwa ziwa, mazi yangu ungekunywa. Kama Mungu anavyopenda wanadamu, mhubiri anavyo penda waumini na mwezi anavyopenda jua kwani humuwezesha kung’aa ndivyo ulivyodhihirisha kama baba wetu wa taifa, unatupenda sisi wanafunzi wa kidigitali. Mwenyezi Mungu akupe mbawazi njema kwa sababu wewe ni wahedi katika mitihani. Asante.